KIUNGO Ladack Chasambi nyota wa Simba anaingia katika orodha ya nyota waliofunga kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 2 2024.
Ni Saido Ntibanzokiza alifungua pazia la utupiaji dakika ya 7, Pa jobe dakika ya 14, Kibu Dennis dakika ya 22.
Mwamba wa Lusaka Clatous Chama aliyekuwa na siku nzuri kazini alifunga bao dakika ya 76, Chasambi aliyeanzia benchi alifunga bao dakika ya 85 na Fabrice Ngoma ilikuwa dakika ya 89.
Mwisho ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 6-0 Jwaneng Galaxy. Wanatinga hatua ya robo fainali ikiwa ni mara ya nne kufanya hivyo na kukomba zawadi ya milioni 30 kutoka kwa Rais Samia Suluhu.
Pointi 9 baada ya mechi 6 vinara ni ASEC Mimosas wenye pointi 11, Timu mbili kutoka Tanzania zinatinga hatua ya robo fainali ikiwa ni Simba na Yanga iliyokuwa kundi D.