Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe baada ya ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Namungo FC, amewataka mashabiki wa Klabu hiyo kutoingia kwenye mjadala wa ubingwa na namna watakavyofanya parade la ubingwa msimu huu.
Kauli hiyo ya Kamwe inakuja ikiwa ni saa chache baada ya aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Manara kuandika kuwa msimu huu Yanga itakuwa Bingwa na itakuwa bingwa mara 10 mfululizo mpaja Rais Samia Suluhu atakapoondoka madarakni mwaka 2023 huku akiwatambia watani zao Simba kuwa Parade la ubingwa la mwaka huu litasimamisha nchi haijawahi kutokea.
“Please Wananchi, tusiingie kwenye huu mtego wa Wachambuzi wasiotutakia mema. How come tujione Mabingwa ikiwa bado tuna mechi 13 zimebaki?
Huu ni tego na msikubali kuuingia kizembe. Ligi Bado sana hii, kunapointi 39 zimebaki. Acheni kabisa stori za ubingwa kwa sasa.
Tufurahi tunaposhinda, tumshukuru Mungu na kisha tuanze maandalizi ya mchezo unaofata kwa umakini na ari kubwa.
Jumatatu ni vs Ihefu Football Club pale Azam Complex.
Focus yetu iwe hapo na sio kuanza mijadala ya Parade kwa sasa. Hizi pointi 3 za Ihefu ni Muhimu sana sana.
We Are Young Africans Sports Club
Mwenyekiti wa Wasemaji Ali Prince Ki Pakamwe.”