MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema wanatambua mchezo dhidi ya Geita Gold hautakuwa mwepesi licha ya kuwa na mwendo mzuri katika mechi zilizopita.

Kocha huyo amebainisha kwamba hawezi kusema kwamba watafunga mabao mengi kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold kwa kuwa yeye hafanyi kazi ya ubashiri.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku ikiwa ni mzunguko wa pili,ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Yanga ilikomba pointi tatu.

Gamondi amesema:”Tumejiandaa vizuri kucheza na Geita Gold, tunafahamu kila mpinzani kuna namna yake ya kujiandaa kimbinu, Ukitazama matokeo yao ya hivi karibuni wameimarika hivyo lazima tuchukue tahadhari ya kutosha bila kujali matokeo yetu ya awali.

“Nina wachezaji wengi wazuri sana, tunaweza kucheza aina yoyote ya mchezo, iwe kushambulia, kumiliki mpira nk. Tunaweza kubadilika badilika kulingana na matakwa ya mchezo kabla na wakati wa mchezo, sijawahi kucheza na aina moja ya falsafa huwa nabadilika kulingana na namna mpinzani anavyocheza na namna navyoweza kumkabili.

“Mechi tatu tumefunga magoli 15, tumeruhusu bao 3, kimsingi hizi ni takwimu bora siwezi kusema kwamba Geita nao tutawafunga magoli mengi huo utakuwa ubashiri sifanyi kazi ya kubashiri, ninachoweza kufanya kwa sasa ni kujiandaa kushinda mchezo. Tumejiandaa kucheza nao kwa namna yoyote ambayo watajipanga, nafikiri watakuja na mbinu za kujilinda lakini hainipi hofu kwa sababu nina vijana wazuri,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here