simba na yanga

Haya ni sehemu ya maoni ya shabiki wa soka aliyeandika kwenye jukwaa la Jamii forum, Huwa sifurahii kuona mafanikio ya Yanga kitu kilichofanya nisiwe naangalia michezo Yao.

Kama bahati mbaya Jana nilikaa peke yangu mbele ya luninga kuangalia mechi ingawa niliumia ila hiki ndio nilichokiona Kwa yanga.

1. Uongozi mzuri unaowapa hamasa wachezaji na benchi la ufundi ndio umeifikisha hapa yanga.

2. Wachezaji wa yanga wanajituma, wakipoteza mpira haraka wanapambana kuutafuta na kuurejesha kwenye himaya Yao.

3. Yanga wamefanya usajili wa maana sana, sifikirii na sidhani kama Kuna kiongozi aliyechukua 10% Ili amlete mchezaji

4. Pacome zouzou ni mtu, Simba SC walifika mapema Ivory coast na wakashindwa kumsajili ( poor leadership).

5. Morali ya timu Iko juu sana, timu inapambama kupata inachokitafuta na ndani ya muda mfupi inakipata, tofauti kabisa na Simba ambayo inacheza bila kujua inatafuta nini ( rejea mechi ya juzi na Asec)

6. Wachezaji wanacheza kitimu na yeyote akionekana hayuko mchezoni anapumzishwa nje ( tofauti na timu yangu ambayo mkalimani saidoo hachezi kitimu na anamaliza dakika zote 90 ).

Mnyonge mnyongeni Yanga SC Iko moto sana.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here