KITAIFA

Nimempa maelekezo Dube, kama atayafuata atatisha sana – Gamondi

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema Prince Dube ni mshambuliaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa, lakini kuna baadhi ya mambo yanamfanya ashindwe kufunga mabao mengi.

Kwa mujibu wa Gamondi mchezaji huyo anatakiwa kuongeza umakini kidogo mbele ya lango la wapinzani ili kuweza kufunga mabao mara kwa mara.

“Tayari nimekaa naye na kumpa maelekezo na kama atayafuata atakuwa miongoni mwa washambuliaji watakaokuwa wakifunga mabao mara kwa mara” alisema Gamondi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button