Kocha wa Bayern Munich ya Ujerumani, Thomas Tuchel ambaye amepanga kuondoka kwa wakali hao mwishoni mwa msimu huu huenda akatua katika timu ya Manchester United kurithi mikoba ya Erik ten Hag ambaye huenda akatimuliwa katika kikosi hicho kama mpaka mwisho wa msimu akiwa hana matokeo mazuri na timu hiyo
Mwekezaji wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe ambaye kipaumbele chake ni kuhakikisha anacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao anataka kusubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kuamua kuhusu mustakabali wa meneja wao Erik ten Hag
Hivyo ili ten Hag apone katika kikombe hichi inambidi aiwezeshe timu hiyo ipate matokeo mazuri