Simba

WAWAKILISHI wa Tanzania Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ngoma ni nzito baada ya kugawana pointi moja na wapinzani wao ASEC Mimosas.

Kwenye mchezo huo wa hatua ya makundi Simba ilikuwa na hesabu za kupata pointi tatu kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao mwsho ubao ukasoma ASC Mimosas 0-0 Simba.

Ngoma ni nzito kwa Simba katika kufanikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali kwa kuwa wapinzai wao Jwaneng Galaxy na Wydad wote wananafasi ya kutinga hatua hiyo ikiwa kila mmoja atashinda mechi zake.

Simba inafikisha pointi sita huku ASEC wakiwa na pointi 11 nafasi ya kwanza, nafasi ya tatu Jwaneng mwenye pointi nne huku Wydad ana pointi tatu nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi B.

Kete ya mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy itaamua nani ataungana na ASEC Mimosas robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa Simba itashinda itakuwa na uhakika wa kutinga robo fainali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here