Wenyeji wa Fainali za Afcon 2023, Ivory Coast imetwaa taji la michuano hiyo mikubwa Afrika baada ya kuifunga Nigeria mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara.

Mabao mawili ya Frank Cassie na Sebastien Haller yaliiwezesha Tembo hao kutwaa ubingwa huo mbele ya Tai ikiwa ni baada ya miaka tisa tangu mara ya mwisho ibebe mwaka 2015.

Mchezo huo ulishuhudiwa na Rais wa nchi hiyo, Alassane Ouattara, Rais wa Shirikisho l Soka Duniani, Gianni Infantino na wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe na Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger na magwiji wa zamani wa timu hizo Nwanko Kanu wa Nigeria, Didier Drogba, Solomon Kalou wa Ivory Coast na wengine.

Ilikuwa ni burudani ya aina yake kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku bahati ikienda kwa Tembo ambao imebeba kwenye ardhi yao ya nyumbani na kuibua shangwe kwa mashabiki wake waliokuwa wengi uwanjani na nchi hiyo kwa jumla.

Fainali hizi zilifunguliwa na kufungwa katika Uwanja wa Alassane Ouattara na nyota wa Ivory Coast waliungana na Rais wa nchi hiyo Ouattara kufurahia ubingwa huo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here