Klabu ya Simba imemtambulisha mshambuliaji Freddy Michael Kouablan ambaye ni raia wa Ivory Coast mwenye miaka 26 ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea ligi kuu ya Zambia kwenye klabu ya Green Eagles

Ambapo ndani ya klabu ya Green Eagles alijiunga nayo mwanzoni mwa msimu wa 2024 akitokea katika klabu kutokea Angola ya Clube Desportivo da Huila.

Huku takwimu za timu aliyotokea ya Green Eagles inaonyesha Hadi sasa Freddy ndiye anaongoza kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu ya Zambia kwa kuwa na magoli 14 na pasi za magoli 4.

Katika Mitandao ya kijamii moja kati ya maswali ambayo wengi wanauliza ni juu ya uhalisia wa umri wa mshambuliaji huyu mpya wa Simba je ni kweli ana hiyo miaka 26, huku wengi wakisema kuwa unaweza ukadhani ni kocha mpya katambulishwa kumbe ni mchezaji. Unaweza weka comment yako katika sokaleo.com

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here