NYOTA Pa Omar Jobe ni mnyama mwingine baada ya kutambulishwa rasmi Januari 15 2024 ikiwa ni usajili wa kuboresha kikosi hicho kilichogotea nafasi ya pili Mapinduzi 2024.

Ipo wazi kwamba Januari 13 ubao wa Uwanja wa New Amaan baada ya dakika 90 kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi ulisoma Mlandege 1-0 Simba.

Joseph Akandwanao aliwakanda Simba kipindi cha pili dakika ya 54 ambapo aliingia akitokea benchi. Simba walipambana dakika zote zilizobaki safu ya ushambuliaji ilikwama kupata bao.

Anakuja kuungana na Jean Baleke kwenye upande wa ushambuliaji ambapo inatajwa kwamba huenda Moses Phiri akapewa mkono wa Thank You ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha.

Wengine ambao wametambulishwa Simba ni Saleh Karabaka, Babacar Saar na Ladack Chasambi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here