HIZI NI TABIA ZA MABINGWA

Simba SC iliyopo nchini Morocco ni Simba ngeni kabisa, Simba hii sio uliyoizoea hii ni kuanzia kwa wachezaji ,viongozi na hata mashabiki … saikolojia zao kuelekea fainali ya huko Morocco na ya marudiano hapa Tanzania ni Tabia ya timu bingwa kwa maana mechi imechukuliwa kikubwa.
Hizi kelele zote za mtandaoni ni za hapa hapa mtandaoni tu na wapiga kelele wengi wataicheki mechi kwenye TV , hofu ni ya waliobaki nyumbani tu lakini waliopo uwanja wa vita hali ni shwari na focus ni fainali
Watu wanapaswa kujua Simba wanajihudumia kwa kila kitu, unaweza kuwa umezaliwa Morocco lakini usijue timu imeweka kambi wapi, sehemu pekee utakayowaona wachezaji ni Airport pekee, hii ni nidhamu iliyotengenezwa ili kuwapa utulivu wachezaji na benchi la ufundi .
Hata Waandishi waliosafiri kwenda Morocco wanapewa ruhusa ya kufanya kazi yao lakini baada ya program za mwalimu kumalizika, maana yake hakuna taarifa ya Simba ya kimbinu ambayo utaipata popote hata kama kuna nzi amejichanganya na kundi la nyuki ogopa wapika stori.
Unaweza kusema Simba wana amani kuliko wenyeji wao Berkane Nitarudi tena kukwambia kwa nini ….. lakini baki na hii ya kuwa Simba wameonesha tabia ya Timu Bingwa na imewatisha wenyeji.