KOCHA Mkuu wa Yanga , Miguel Gamondi ameonekana bado anahitaji kuwa makini mbele ya Simba kwa kutumia muda wa kutazama michezo yote mikubwa waliocheza wapinzani wao hivi karibuni.
Hatua hiyo kuelekea katika mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Wekundu wa Msimbazi hao kwa kuhitaji msimu huu kuvuna alama zote sita zile za mzunguko wa kwanza walizoshida bao 5-1 na Jumamosi hii kutafuta ushindi.
Yanga watakuwa wenyeji ikiwakaribisha Simba mchezo huo utakaochezwa Jumamosi hii katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam, saa 11:00 jioni.
Kocha huyo ameamua kukaa na wachezaji kupitia michezo mbalimbali ili kuweza kila mmoja anawezaje kufanya majukumu yake.
Kwa mujibu wa Gamondi kuwa licha ya Simba kutokuwa vizuri hivi karibuni lakini mpinzani wake huyo amekuwa hatari hasa katika mechi kubwa na kumlazimi kuanza kufatilia na kuona ubora wao.
Amesema ameona uimara wa safu ya ushambuliaji, viungo na ulinzi kwa wapinzani wake ikiwrmo kwenye upigaji wa mipira ya vichwa na kutakiwa kufanyia kazi kila idara mapema kabla ya mchezo huo.
“Tumekuwa tukifanya vizuri katika hizi mechi, mchezo wa Derby ni tofauti na michezo tuliyocheza kwa sababu ni muhimu kwa kila timu, tunafanyia kazi ubora wa Simba lakini pia mapungufu yetu.
Tunahitaji kutumia vizuri nafasi, tumekuwa tukipata nafasi nyingi tunazotengeneza lakini tunashindwa kuzitumia hasa kulingana na umakini wa safu ya ushambuliaji,” amesema Kocha huyo.
Ameongeza kuwa kabla ya kumvaa mpinzani unaangalia ni jinsi gani ya kuweza kumkabili, kwa muda ambao wameutumia kuisoma Simba naimani kila mmoja ametambua kuwa wanaenda kukutana na timu ya aina gani.
“Simba ni timu bora, hii mechi ina presha ya mashabiki, viongozi, benchi la Ufundi na wachezaji naamini kila mmoja anajiandaa anavyoweza kuweza kuonesha mchezo mzuri,” amesema.
Amesema anawaamini wachezaji wake kwamba wanauwezo wa kupambana kuhakikisha wanapata pointi tatu katika mchezo huo ili kuendelea kuwa katika mipango yao ya kutetea ubingwa.
Katika hatua nyingine Ofisa habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Tanzania, Kareem Boimanda amesema maandalizi ya mchezo huo namba 180 kati ya Yanga dhidi ya Simba jumamosi yanaendelea vizuri.
Amesema suala la ulinzi na usalama hilo halina mashaka yoyote kila kitu kutaenda sawa, kutakuwa na vizuizi ambavyo itapunguza msongamano karibu na uwanja.
“Baadhi ya njia zitafungwa ikiwemo barabara ya DUCE na huku wakitakuwa kutumia barabara ya Taifa na magari yatakayoruhusiwa kupita njia hiyo ni yale yenye stika maaalum ambayo yataingia uwanjani,” amesema Boimanda.
Meneja wa masoko wa NBC, David Raymond ameweka mipango yao kuelekea mchezo wa Derby pamoja kuelekea mwishoni mwa msimu huu ambapo wanatarajia kukabidhi basi moja ya timu inayoshiriki Ligi hiyo.