KITAIFA

SIMBA KAMILI KUKUPIGA NA BERKANE KESHO MAY 17

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wao dhidi ya RS Berkane unaotarajiwa kuchezwa Mei 17 2025.

Tarai kikosi cha Simba SC kipo nchini Morocco kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo na ule wa pili unatarajiwa kuchezwa Tanzania.

Awali mchezo wa fainali ya pili ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ila taarifa kutoka CAF zimeeleza kuwa mchezo huo unapaswa kuchezwa Zanzibar, Uwanja wa New Amaan Complex ambapo Simba SC wameweka wazi kuwa taarifa ya uwanja wa mchezo utatangazwa mara baada ya mchezo wa kwanza kukamilika.

Kuhusu mchezo wa fainali ya kwanza Ahmed ameweka wazi kuwa watafanya kazi kubwa kutafuta matokeo ili kupambania malengo ya kutwaa taji hilo kubwa Afrika.

“Tupo vizuri na tunatambua kwamba mchezo wetu dhidi ya RS Berkane utakuwa mgumu, kikubwa ni kuona tunapata matokeo katika mchezo wetu ili kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa wa Afrika.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu na benchi la ufundi linafanya kazi yake kuona kwamba tunapata matokeo mazuri, tupo tayari na tutapambana ili kupata ushindi kwenye mchezo wetu ugenini, ikishindikana basi hata sare ili kazi tuimalize nyumbani.”

Kauli mbiu ya Simba SC kuelekea kwenye mchezo wa hatua ya fainali inasema TUNABEBA.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button