KITAIFA

Tanzania Vs Sudan Leo 03/11/2024 Saa Ngapi?

Tanzania Vs Sudan Leo 03/11/2024 Saa Ngapi?

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania, almaarufu kama Taifa Stars, leo itakua na kibarua cha kulipiza kisasi dhidi ya Sudan katika mchezo wa marudiano wa kuwania nafasi kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) mwaka 2025. Mchezo huu unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, na unatoa fursa kwa Stars kusonga mbele katika hatua za pili za mashindano haya baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Sudan kwa bao 1-0.

Tanzania Vs Sudan Leo 03/11/2024 Saa Ngapi?

Ratiba na Mahali pa Mchezo wa Tanzania Vs Sudan Leo

Mchezo huu wa marudiano kati ya Tanzania na Sudan utafanyika leo, 03 Novemba 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Mashabiki na wapenzi wa soka watakuwa na nafasi ya kufuatilia moja kwa moja kupitia televisheni na mitandao ya kijamii, huku wengi wakitarajia matokeo chanya kutoka kwa Stars.

Kiingilio na Maandalizi ya Mashabiki

Wapenzi wa soka nchini wamepewa nafasi ya upendeleo kwa mchezo wa leo, ambapo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuwa hakuna kiingilio kwa wataoingia uwanjani kuiunga mkono timu yao.

Hii ni hatua inayolenga kuongeza hamasa na kuhakikisha Stars inapata sapoti ya kutosha ili kufanikisha malengo yake. Matarajio ni kwamba uwanja utajaa mashabiki wenye shauku kubwa ya kuona Stars ikiibuka na ushindi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button