Baada ya jana klabu ya Al Nassr kupata sare ya 1-1 dhidi ya Al Raed kwenye ligi kuu Saudia nahodha wa timu hiyo na mshindi mara 5 wa tuzo ya Ballon D’or Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kufunga mabao mengi kuliko idadi ya mechi kwenye ligi huiyo tangu ahamie Saudia.
Hadi sasa kwenye ligi hiyo Ronaldo amecheza michezo 48 na kufanikiwa kufunga magoli 50, ikiwa ni mchezaji wa kwanza kufanya hivyo mapema.