KIUNGO wa kazi ndani ya Yanga Farid Mussa ameweka wazi kuwa wanafanya kazi kwa ushirikiano kufikia malengo ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi.
Ipo wazi kuwa kwa 2024/25 Gamondi amekiongoza kikosi cha Yanga katika mechi mbili za ushindani ambazo ni dakika 180 kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kushinda mechi zote mbele ya washindani wake uwanjani.
Mchezo wa kwanza ilikuwa Yanga 1-0 Simba nusu fainali ya pili na Azam FC 1-4 Yanga fainali zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa hivyo Farid anaingia kwenye orodha ya mastaa walianza kuvaa medali na kutwaa taji mwanzo wa msimu.
Farid alikuwa anavaa uzi namba 17, 2023/24 atatumia namba 12 msimu wa 2024/25 baada ya kubadilishana na Clatous Chama aliyeibuka hapo akitokea Simba.
Kiungo huyo amesema: “Tunafanya kazi kwa ushirikiano sisi ni timu na malengo yetu ni kupata matokeo mazuri katika mechi zetu zote.”
Kwa upande wa Gamondi ameweka wazi kuwa wanacheza kwa umakini kwenye mechi zao zote ili kupata matokeo mazuri uwanjani kutokana na ushindani uliopo na wachezaji kuwa makini kufuata maelekezo.