Klabu ya Kengold iliyopanda ligi kuu msimu huu itacheza mchezo wao wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya klabu ya Singida Black Stars kwenye dimba la Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya siku ya Agosti 18.
KenGold ilipanda daraja kwa rekodi nzuri kwa kutopoteza mchezo wowote wa nyumbani kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya kwenye Championship na kutwaa ubingwa wa jumla wa ligi hiyo na sasa kazi inahamia Ligi Kuu.