Klabu ya Namungo FC almaarufu ‘Wauaji wa Kusini’ leo August 16, 2024 imetambulisha jezi mpya zitakazotumika kwenye msimu wa 2024/2025 ambapo jezi hizo ziko kwenye seti 5 ambayo zitatumika kwenye michuano ya nje, ndani na ya Kimataifa.
Jezi hizo zimetambulishwa kwenye Hoteli ya Ruangwa Pride iliyoko Ruangwa Mkoani Lindi na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu bara msimu wa 2024/25 imesema jezi hizo zitaanza kuuzwa na kupatikana kwenye maduka yote ya vifaa vya michezo Nchini.