KITAIFA

BAADA YA KUONA GUEDE ANAVYOCHEZA, KIEMBA KAGUNA WEEE..KISHA AKASEMA HILI

Mchezaji wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Amri Kiemba amesema kuwa atatoa maoni yake kuhusu mshambuliaji mpya wa Yanga, Joseph Guede mawisho wa msimu kwani kwa sasa bado ni mapema sana.

Kauli hiyo ya Kiemba inakuja baada ya mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Yanga katika dirisha dogo kucheza mechi tano bila kufunga wala kutoa pasi ya mwisho ya bao jambo ambalo limeibua mijadala kuwa huenda uwezo wake ni mdogo.

“Joseph Guede usajili mpya Yanga katika dirisha dogo katika nafasi ya ushambuliaji, mwamba bado hajafunga goli hata moja ila kimpira huu sio wakati sahihi kuanza kusema Guede ni mali au sio mali.

“Bahati mbaya aliyoipata Guede ni kwamba kaja katika timu ambayo ina matarajio makubwa kwake kuliko kawaida hususani mashabiki, hata kama Viongozi, Mashabiki wa Yanga hawasemi hadharani ila ukweli wanatamani kuona wamepata mbadala wa Mayele kwa haraka.

“Mshambuliaji yoyote wa sasa anayekuja Yanga wengi wanatamani kuona awe kama Mayele au zaidi ya Mayele ila akija kama average player bado atakuwa na wakati mgumu sana Yanga. Kwa Guede binafsi nitaanza kuwa na maoni zaidi mwisho wa msimu kuhusu uwezo wake,” amesema Kiemba.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button