Kocha mkuu wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola akizungumza kuhusu Haaland baada ya mechi ya jana dhidi ya Chelsea amesema kuwa mshambuliaji huyo anafanana kitakwimu na washindi mara nyingi ya tuzo ya Ballon D’or Lionell Messi na Cristiano Ronaldo.
“Hizi namba ni kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni namba za kiwango hicho. Kufanya anachofanya Haaland hapa England ni jambo la kushangaza.”
Haaland ndiye mchezaji aliyeifungia Man City goli la kwanza la msimu 2022/23 akafanya tena 2023/24 na jana tena 2024/25 huku goli lingine la Man City likifungwa na kiungo Mateo Kovacic.