TETESI ZA USAJILI SIMBA SC 2024/2025

TETESI Za Usajili Simba SC 2024/2025, Tetesi Za Usajili Simba Dirisha Kubwa la Usajili 2024/2025, Usajili Simba 2024,Tetesi za Usajili Simba Dirisha Kubwa la usajili 2024/2024.

Debora Fernandes Mavumbo Simba SC
Klabu ya Simba ipo Katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo, Debora Fernandes Mavumbo kutoka Mutondo Stars ya kwao Zambia Kwa mkataba wa miaka miwili.

Nathan Fasika Idumba Simba SC
Klabu ya Simba imefanya mazungumzo na wawakilishi wa mlinzi wa kimataifa wa Congo DR, Nathan Fasika Idumba mwenye umri wa miaka 25.
Fasika ambaye kwa sasa anaitumikia Valerenga ya Norway kwa mkopo akitokea Cape town City ya Afrika Kusini, sio mara ya kwanza Simba kujaribu kumsajili mchezaji huyo.

Aubin Kramo Kouamé Simba SC
Winga wa Simba, Aubin Kramo Kouamé mwenye umri wa miaka 25 ataendelea kuwa sehemu ya Kikosi Cha simba msimu ujao wa 2024/2025 baada ya kupona majeraha.

D’Avila Messi Kessie Simba SC
Wakati viongozi wa Simba wakihaha kukisuka upya kikosi hicho kwaajili ya msimu ujao, tayari wameanza kumpigia hesabu winga raia wa Ivory Coast, D’Avila Messi Kessie ambaye inaelezwa huenda mambo yakienda sawa atajiunga na miamba hiyo.
D’Avila mzaliwa wa January 20-2024 kwa sasa anakipiga Inova Sporting Club Association ya Ivory Coast, huku nyota huyo akisifika kwa uwezo wa kucheza winga zote ambapo msimu uliopita alifunga mabao 11 huku akitoa pasi za mabao 6.

Ayoub Lakred Simba SC
Klabu ya Simba imepanga kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja hadi 2025 golikipa wake, Ayoub Lakred raia wa Morocco mwenye umri wa miaka 28.

Augustine Okejepha Simba SC
Klabu ya Simba ilituma ofa ya USD 200,000 katika klabu ya Rivers Utd ikihitaji saini ya kiungo wa ulinzi, Augustine Okejepha lakini ofa hiyo inatajwa ni ndogo na wanahitaji USD 270,000 ili kumuachia Okejepha mzaliwa wa April 14-2004 nchini Nigeria.

Rahim Shomary Simba SC
Uongozi wa Simba umeanzisha mazungumzo ya kumpata beki wa kushoto wa KMC FC, Rahim Shomary mwenye umri wa miaka 19 kwaajili ya kuiongezea nguvu timu hiyo Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.

Damaro Camara Simba SC
Klabu ya Simba imeanza mazungumzo ya kuinasa Saini ya kiungo mkabaji anayeweza kucheza kama beki wa kati, Damaro Camara mwenye umri wa miaka 20 kutoka Hafia ya kwao Guinea.

Joshua Mutale Simba SC
Klabu ya Simba ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa winga, Joshua Mutale mwenye umri wa miaka 22 kutoka Power Dynamos ya kwao Zambia.

Valentin Nouma Simba SC
Klabu ya Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo, Valentin Nouma raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 24 kwaajili ya kuipata huduma yake Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.

Joyce Lomalisa Simba SC
Mbali na Nouma, Simba pia awali ilitajwa kuwa kwenye mazungumzo na beki, Joyce Lomalisa aliyemaliza mkataba ndani ya Yanga ambapo timu hiyo inaangalia uwezekano wa kumpata beki wa kushoto aende kusaidiana na Mohamed Hussein.

Salum Athuman ‘Stopper’ Simba SC
Klabu ya Simba inajaribu kufanya mazungumzo ya kumsajili beki wa KVZ ya Zanzibar, Salum Athuman ‘Stopper’ ambaye amekuwa na kiwango bora.

Yannick Bangala Azam FC
Viongozi wa Simba wametajwa kufanya mawasiliano na wakala wa kiungo, Yannick Bangala anayeichezea Azam FC ili kuangalia uwezekano wa kumpata nyota huyo wa zamani ya Young Africans.

Brian Mandela Onyango Simba SC
Klabu ya Simba inamuwania beki wa kati wa Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini raua wa Kenya, Brian Mandela Onyango mwenye miaka 29.

Samwel Onditi Simba SC
Klabu ya Simba imefanya mawasiliano na wawakilishi beki, Samwel Onditi wa Geita Gold, kwaajili ya Kuangalia uwezekano wa kumsajili beki huyo mwenye uwezo wa Kucheza kama beki na kiungo wa kati ambaye kwa sasa ni mchezaji huru

Steve Komphela Simba SC
Klabu ya Simba ipo kwenye Mazungumzo ya mwisho na Kocha Steve Komphela mwenye umri wa miaka 56 kutoka Afrika Kusini ili arithi mikoba ya iliyoachwa na Kocha Abdelhack Benchikha.

Serge Pokou Simba SC
Klabu ya Simba inatajwa kuwa Katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo, Serge Pokou mwenye umri wa miaka 23 kutoka ASEC Mimosas ya kwao Ivory Coast kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh200mil.

Kenneth Semakula Simba SC
Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na aliyekuwa kiungo wa SC Villa ya Uganda, Kenneth Semakula ili kujiunga nao msimu ujao.

Derrick Mukombozi Simba SC
Uongozi wa Simba SC upo kwenye mazungumza ya kunasa saini na beki wa Namungo na timu ya taifa ya Burundi, Derrick Mukombozi kwaajili ya kuziba pengo la Henock Inonga ambaye anatajwa kutaka kuondoka klabuni hapo.

Elie Mpanzu Simba SC
Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano ya kumsajili winga wa kulia wa kimataifa wa DR Congo na klabu ya AS Vita Club, Elie Mpanzu mwenye umri wa miaka 22 kwa Mkataba wa miaka miwili.
Inaelezwa kuwa Klabu ya Simba SC ipo kwenye mipango ya kumsajili Mshambuliaji, Agostinho Cristóvão Paciência maarufu ‘Mabululu’ raia wa Angola kutoka Al Ittihad Alexandria ya Misri.
Mabululu mwenye umri wa miaka 31 amefunga magoli jumla ya mabao 10 kwenye mechi 16 za Egyptian Premier League msimu huu.
Klabu ya Simba imetajwa kuwa ipo mbioni kuwasajili Wachezaji wawili wa Hafia FC ya Guinea, Mohamed Damaro Camara mwenye miaka 21 na Ousmane Fernandez ‘Drame’ mwenye umri wa miaka 23.
Wachezaji hao wanatajwa kuja kuchukua nafasi ya Sadio Kanoute anayedaiwa kuomba kuondoka mwishoni mwa msimu pamoja na Fabrice Ngoma.
Usajili huo umetajwa ni kwaajili ya kuimarisha eneo la kiungo, ambapo Camara anacheza nafasi ya kiungo mkabaji, huku Drame akiwa na uwezo wa kucheza namba sita pamoja na namba nane.

Fiston Kalala Mayele Simba SC
Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ Kupitia A-fm Radio amesema kuwa wametuma maombi kwenye Klabu ya Pyramids FC ya nchini Misri ya kumpata Kwa Mkopo aliyekuwa Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele.
Klabu ya Simba imefikia Makubaliano ya kumnunua beki wa kati, Lameck Lawi kutoka Klabu yake ya Coastal Union ya Tanga.
Uongozi wa klabu ya Simba umepanga kupiga hodi kwenye klabu ya Azam kwaajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ayoub Lyanga, imefahamika.
Mkataba wa Lyanga na Azam unafikia mwishoni mwa msimu huu na tayari mabosi wa Azam wameanzisha mazungumzo ya kumuongezea mkataba licha ya Simba nao kuweka dau lao mezani kwa nyota huyo.

Yusuph Kagoma Simba SC
Kiungo, Yusuph Kagoma yupo mbioni kujiunga na klabu Simba SC akiwa Mchezaji huru baada ya kuachana na Singida Fountain Gate FC.

Pa Omar Jobe Simba SC
Klabu ya Simba huenda ikaachana mshambuliaji wake, Pa Omar Jobe mazungumzo yanakaribia kukamilika.

Saido Ntibanzonkiza Simba SC
Kiungo wa klabu ya Simba SC, Saido Ntibanzokinza raia wa Burundi ameachana rasmi na Klabu hiyo.