KITAIFA

KUZIONA SIMBA NA YANGA NI “BUKU TANO TU”

Viingilio vya mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba maarufu kwa jina la ‘Kariakoo Derby’ ambao utachezwa Jumamosi ya Aprili 20, 2024 vimewekwa wazi huku kiingilio cha chini kikiwa ni Sh5,000.

Viingilio hivyo vimetangazwa kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Ligi Kuu Tanzania Bara huku ikiwa imesalia wiki moja kabla ya mchezo huo ambao utachezwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa.

Viingilio hivyo ni kama ifuatavyo.

VIP A – Sh 50,000
VIP B – Sh 30,000
VIP C – Sh 20,000
Orange – Sh 10,000
Mzunguko – Sh 5,000

Mara ya mwisho watani hao wa jadi walipokutana katika ligi, Simba ilikumbana na kipigo cha mabao 5-1 hivyo mchezo huu utakuwa wa kisasi, heshima na vita ya kupigania ubingwa wa ligi ambayo Yanga inaongoza ikiwa na pointi 52, Azam inashika nafasi ya pili (47) huku Mnyama akiwa pointi 46.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button