Wakati kikosi cha Simba kikiendelea kutakata kwenye Ligi Kuu, beki wa timu hiyo, Che Malone Fondoh, amezidi kuwa mtu muhimu kwenye eneo la ulinzi, akionekana hana presha kabisa.

Awali Malone alikuwa akicheza na Enock Inonga Baka kama mabeki wa kati, lakini Mkongo huyo aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kushiriki Afcon 2023 na kukosa michezo ya Kombe la Azam Federation dhidi ya Tembo na Simba haikuruhusu bao, pamoja na mechi nne za Ligi Kuu Bara huku akiiongoza vyema safu ya ulinzi.

Beki huyo raia wa Cameroon, aliyetua Simba msimu huu akitokea Cotton Sports, amekuwa panga pangua ya makocha wote waliowahi kufundisha timu hiyo, kuanzia Mbrazili Robertinho Oliviera na sasa Abelhack Benchikha na kinachombeba ni kuwa bora kila anapobadilishiwa pacha wa kucheza naye.

Kuanzia michuano ya ASFC, Inonga aliyokosekana, Malone amebadilishiwa mabeki wa kucheza naye katikati lakini ubora wake umezidi kuwa juu.

Beki huyo amecheza na Kennedy Juma na Hussein Kazi na kutokana na uwezo wake mzuri wawili hao hawakupata wakati mgumu. Katika michezo minne ya ligi aliyokosekana Inong, timu hiyo imeonyesha kiwango kizuri ikiruhusu bao moja tu katika sare ya 1-1 na Azam FC, lakini ikiwa imefunga mabao saba iliposhinda dhidi ya Geita, Mashujaa na Tabora United. Bao hilo lililofungwa na mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube dakika ya 13, Che Malone muda huo alikuwa uwanjani akicheza pacha na Hussein Kazi, huku Kennedy akiwa benchi na kuingia kipindi cha pili.

Kazi na Kennedy wamecheza dakika 460, Kennedy akiwa kinara akitumika 225 na Kazi 135, kwenye michezo minne.

Inonga ambaye alikuwa panga pangua kwenye michezo ya mwanzoni ya Simba akicheza na Che Malone, waliruhusu mabao 13 kwenye michezo 10 ya ligi wakiwa pamoja.

Hii ni safu ya ulinzi ambayo inashika nafasi ya tano kwa kuruhusu mabao machache, namba moja inashikwa na Yanga ambayo imefungwa nane, Azam imeruhusu mabao 11, Namungo 12 huku Costal Union nayo ikiwa imefungwa mabao 11.

Hata hivyo, kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa wastani wanapocheza Inonga na Che Malone au wanapocheza mabeki wengine kwenye nafasi hiyo, kwa kuwa kwenye wastani wawili hao wanaonekana kuruhusu mabao mengi zaidi.

Akizungumzia safu hiyo baada ya mchezo dhidi ya Azam, Benchikha alisema: “Simba haikucheza vizuri kwenye eneo la ulinzi kulikuwa na makosa ambayo yanazuilika.

“Angalau kipindi cha pili mambo yalikuwa tofauti lakini mwanzoni tulikuwa na makosa mengi sana ya kiulinzi.

Katika michezo minne Che Malone ni beki pekee katika safu hiyo ya ulinzi aliyecheza dakika zote 360 huku wengine wakipokezana.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here