Chama- Ndoto ya Ubingwa wa Afrika na Yanga Inawezekana!
Klabu ya Yanga imekuwa ikiimarika kwa kasi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na kiungo mshambuliaji Clatous Chama ameweka wazi ndoto yake ya kutwaa ubingwa huo akiwa na klabu hiyo.
Chama, ambaye amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha Yanga, amesema kuwa ndoto yake kubwa ni kuona Yanga ikitwaa ubingwa wa Afrika na kuvaa medali za ushindi. Ameongeza kuwa anaamini ndoto hiyo inawezekana kutokana na ubora wa timu kwa sasa.
“Ndoto yangu kwenye michuano ya CAF ni kuchukua ubingwa wa klabu bingwa Afrika ukiacha kuwa Mfungaji Bora CAF ndoto yang kubwa ni kuchukua ubingwa wa Afrika,” alisema Chama.
Kiungo huyo ameongeza kuwa, “Kuvaa medali za ubingwa CAF nikiwa Yanga inawezekana kwasababu kama tunavyoona sasa hivi timu iko vizuri sana na natamani sana timu ifike finali na tutimize hiyo ndoto kama timu, ni kitu kikubwa kushinda ligi ya mabingwa.”
Kauli ya Chama inaonyesha dhamira na ari ya wachezaji wa Yanga katika michuano ya mwaka huu. Mashabiki wa Yanga wamekuwa na matumaini makubwa ya kuona timu yao ikifanya vizuri na kufikia hatua ya fainali.
Je, Yanga ina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Afrika?
Yanga imekuwa ikionyesha kiwango bora katika michuano ya mwaka huu, na wamefanikiwa kuitoa klabu kubwa ya TP Mazembe katika hatua ya awali. Hii inaonyesha kuwa Yanga ina uwezo wa kushindana na timu kubwa barani Afrika.
Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa mbele yao. Yanga itahitaji kuendeleza kiwango chao bora na kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika michezo ijayo.