tetesi za soka ulaya

Manchester United inamruhusu Bruno Fernandes kuanzisha mazungumzo ya kuchezea Saudi Arabia, Kevin de Bruyne wa Manchester City anakubali kuhama Al-Ittihad, huku Arsenal wakikubali mkataba wa Riccardo Calafiori.

Manchester United imempa kiungo Bruno Fernandes, 29, ruhusa ya kuanza mazungumzo na Saudi Arabia, huku klabu mbili za Ligi ya Saudia zikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno. (TeamTalk)

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, 33, “amekubali kwa maneno” kujiunga na klabu ya Saudi Arabia Al-Ittihad , na sasa ni juu ya mabingwa hao wa Premier League kuidhinisha kuondoka kwa Mbelgiji huyo. (TeamTalk)

Liverpool wanatumai fowadi wa Misri Mohamed Salah, 32, atasaini mkataba mpya mkataba wake wa sasa utakapokamilika 2025. (Mirror).

Leicester City wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa Fulham Bobby de Cordova-Reid, huku Mjamaica huyo mwenye umri wa miaka 31 akitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. (Telegraph – subscription required)

Kiungo wa kati wa Aston Villa Philippe Coutinho atarejea katika timu ya utotoni ya Vasco da Gama “mara moja” baada ya mazungumzo marefu kuhusu iwapo kandarasi ya Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 32 inaweza kusitishwa. (Birmingham Live)

Arsenal wamekubali mkataba wa beki wa Italia na Bologna Riccardo Calafiori hadi mwaka 2029, lakini vilabu hivyo bado vinahitaji kukubaliana ada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Fabrizio Romano)

West Ham wana nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Villarreal Alexander Sorloth, 28, lakini raia huyo wa Norway ana kipengele cha kumruhusu kuondoka chenye thamani ya karibu £32m katika klabu hiyo ya La Liga. (AS – in Spanish)

Dau la Chelsea la pauni milioni 42 la kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid Samu Omorodion, 20, limekataliwa kwani klabu hiyo inataka angalau pauni milioni 70 kumnunua Mhispania huyo. (Sun)

Arsenal wanajiandaa kumuuza mshambuliaji wa Demark wa Chini ya miaka 21 Mika Biereth, 21, kwa £4m kwa klabu ya Sturm Graz ya Austria.(Standard)

Luton Town , Oxford United na Bristol City zote zina nia ya kumchukua fowadi wa Tottenham mzaliwa wa Ireland Kaskazini Jamie Donley, 19, kwa mkopo wa msimu ujao. (Football Insider)

Manchester United , Crystal Palace na Tottenham Hotspur ni miongoni mwa klabu zinazovutiwa na kiungo wa kati wa Hull City Muingereza Jaden Philogene, 22. (TeamTalk)

Barcelona wanafikiria kumnunua tena beki wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 Emerson Royal kutoka Tottenham Hotspur . (Mundo Deportivo – in Spanish)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here