KITAIFATETESI ZA USAJILI
SIMBA KUMSHUSHA ‘MOUSSA CAMARA’ KUWA MBADALA WA LAKRED
Moussa Camara Kusajiliwa Simba
Zikiwa bado zimesalia wiki chache kufungwa kwa dirisha la usajili na kuanza msimu mpya wa 2024/2025 bado timu mbali mbali zikiendelea kufanya sajili za wachezaji ilikuboresha vikodi vyao.
Ndani ya Timu ya Simba, Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa kipa Moussa Camara ameanza safari ya kuja Tanzania kumalizana na Simba SC siku kadhaa zijazo.
Nyota huyo raia wa Guinea atajiunga na Simba SC kuchukua nafasi Ayoub Lakred ambae amepata majeraha ya muda mrefu.