Simba na azam

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Mei 9 2024 uongozi wa Simba umebainisha kwamba bado haujamaliza.

Simba ipo chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda ina kazi yakusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Azam FC ambao nao wanazihitaji pointi tatu pia.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, ubao ulisoma Simba 1-1 Azam FC hivyo waligawana pointi mojamoja.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano amebainisha kwamba wanatambua ushindani uliopo na wanahitaji kupata pointi tatu muhimu.

“Tunahitaji kupata pointi tatu kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam FC kikubwa ni kupata pointi tatu muhimu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi katika mchezo wetu.

“Wapinzani wetu tunawaheshimu kutokana na kila mmoja anatambua kwamba kila mchezaji yupo tayari kwa kuwa wanatambua umuhimu wa kupata matokeo mazuri,”.

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 53 huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili na pointi 57 kibindoni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here