wababe

WABABE wanne ndani ya CRDB Federation Cup safari imekamilika tayari kwa kila timu kutambua mpinzani wake hatua ya nusu fainali.

Yanga ni mabingwa watetezi wa CRDB Federation Cup walipenya hatua ya nusu fainali kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Yanga 3-0 Tabora United. Yanga hatua ya nusu fainali itakuwa dhidi ya Ihefu.

Azam FC walikuwa nyumbani Mei 3 2024 dhidi ya Namungo FC kwa kupata ushindi wa mabao 4-0 Namungo.

Namungo wamefungashiwa virago wakigotea hatua ya robo fainali hivyo Azam FC itakutana na Coastal Union katika mchezo wa robo fainali ilipata ushindi dhidi ya Geita Gold bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Azam FC mabao yao kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex yalifungwa na Kipre Junior, Idd Nado, Feisal Salum na Gibrill Sillah huku lile la Namungo likifungwa na Ayoub Semtawa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here