AZIZ KI kiungo mshambuliaji wa Yanga kahusika kwenye mabao 23 ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex, Mei 8 2024 ukisoma Yanga 1-0 Kagera Sugar alitoa pasi moja ya bao.
Ilikuwa ni dakika ya 83 pasi hiyo alitoa na kumpa mwamba Mudathir Yahya ambaye aliingia kwenye mchezo huo akitokea benchi.
Yanga inajikita namba moja ikiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 26 msimu wa 2023/24 ambao unakaribia kugota mwisho.
Yanga safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 57 kinara ni Aziz KI mwenye mabao 15 na pasi saba za mabao.
Katika mabao hayo ambayo amefunga ametumia mguu wa kulia kufunga mabao mawili na mguu wa kushoto kufunga mabao 13.