Klabu ya CBE FC inajulikana kama Commercial Bank of Ethiopia , msimu huu ndio mara ya kwanza kushiriki michuano ya CAF CHAMPIONS LEAGUE .
Hii miamba ya CBE ilianzishwa mwaka 1982 , miaka 42 mpaka sasa kwenye historia ya kuanzishwa kwa klabu hii na makao yao makuu yapo Adis Ababa ….. Msimu uliopita walifanikiwa kuwa mabingwa wa ligi ya Ethiopia 🇪🇹.
Klabu ya CBE wamefanikiwa kushiriki miachuano ya CAF CONFEDERATION CUP mwaka 2005 na 2010 ndani ya mara zote walitolewa hatua ya kwanza .
Wanakutana na klabu Yanga baada ya kuwatoa wababe kutoka ligi ya Uganda 🇺🇬 Villa kwa Agg ya 3-2 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza .