KLABU ya Azam imefikia makubaliano na klabu ya Stade Malien (Mali) kumsajili kiungo mshambuliaji, Franck Tiesse. kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia msimu ujao wa 2024-25.
Tiesse (26) anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kushambulia kwa kasi na uwezo wa kutumia miguu yote miwili, akiwa Stade Malien aliisaidia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Nyota huyo raia wa Mali anamudu kucheza kama winga wa kulia, kiungo mshambuliaji na winga wa kushoto.