KITAIFA

YANGA ILITUMIA ‘MIL 206’ KUWAFUATA MAMELODI

Rais wa Klabu ya Yanga Engineer Hersi Said ameeleza gharama ya safari ya timu hiyo kwenda Afrika Kusini kwenye mechi ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns iliyochezwa siku ya Ijumaa.

Hersi akiongea na waandishi habari amesema safari yao iligharimu Dola za Kimarekani 80,000 (Tsh Milioni 206)

“Ni gharama sana kuendesha klabu ya mpira wa miguu. Ninaweza kukuambia safari yetu ya kwenda Afrika Kusini kucheza na Mamelodi iligharimu USD 80,000” — Amesema Hersi

“Tiketi ya kwenda na kurudi (kwa mtu mmoja) ni USD 600. Na nimekuja na watu 50. Hiyo ni USD 30,000. Watu 50 mara USD 150 kwa siku, zidisha kwa siku nne. Hiyo ni USD 30,000 nyingine.

“Hapo hujanunua kitu chochote na gharama za hoteli. Unatakiwa kuzunguka hapa na pale. Baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi wanatakiwa kupewa posho wanaposafiri.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button