tetesi za soka

Liverpool na Bayern Munich wanatathmini upya mipango yao baada ya kocha Xabi Alonso kuamua kusalia Bayer Leverkusen, huku Barcelona wakitazamia kukamilisha dili la kumnunua kocha wa Sporting Lisbon Ruben Amorim kama mbadala wa Xavi anayeondoka. (Independent)

Hata hivyo, bodi ya Barcelona inataka kumshawishi Xavi kuondoka na inamtaka abaki Nou Camp. (Athletic – Usajili unahitajika)

Arsenal wamewasiliana na Bayern Munich kuhusu uhamisho wa kiungo wao wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, lakini wameambiwa mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hautajadiliwa hadi msimu wa joto. (Football transfers)

Arsenal pia wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Sociedad Mhispania Martin Zubimendi, 25, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Bayern Munich. (Caught offside)

Manchester City na Liverpool wanatarajia juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 20, yatatatizwa na uamuzi wa Xabi Alonso kusalia na katika klabu hiyo ya Bundesliga. (HITC)

Manchester United imewajumuisha wachezaji Jarrad Branthwaite,21, wa Everton, Aaron Anselmino ,19, wa Boca Juniors na mchezaji wa kimataifa wa Senegal Mikayil Faye kwenye orodha yao ya kuimarisha safu ya ulinzi msimu huu. (Mail)

Jadon Sancho, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Borussia Dortmund, anaweza kupata fursa nyingine Manchester United ikiwa klabu hiyo itamteua Jason Wilcox wa Southampton kama mkurugenzi wao wa soka. Wilcox alifanya kazi na mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 katika chuo cha soka cha Manchester City. (Manchester Evening News)

Manchester United wana nia ya kumteua meneja wa Ipswich Kieran McKenna kama kocha wao mpya. Raia huyo wa Ireland Kaskazini, 37, aliwahi kufanya kazi katika klabu hiyo kama kocha msaidizi chini ya Jose Mourinho na Ole Gunnar Solskjaer. (Football Insider)

Real Madrid ingependa kumsajili beki wa kati wa Lille Leny Yoro, 18, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Manchester United, Liverpool na Chelsea – msimu huu baada ya Mfaransa huyo kuiambia klabu yake kuwa anataka changamoto mpya. ( Athletic- Usajili unahitajika)

Tottenham huenda ikalazimika kumuuza mlinzi wa Brazil Emerson Royal, 25, ili kusaidia fedha za uhamisho wao katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Leeds United na England chini ya umri wa miaka 21 na beki wa kulia Archie Gray, 18, anatazamwa na Real Madrid na Bayern Munich pamoja na timu nyingi za Ligi kuu ya England. (HITC)

Beki wa Barcelona na Uhispania Marcos Alonso, 33, yuko kwenye mazungumzo ya ya ngazi ya juu na Atletico Madrid kuhusu kujiunga kwa uhamisho wa bila malipo msimu huu wa joto. (Cadena Ser – kwa Kihispania)

Birmingham wako kifua mbele, kumsajili beki wa Queen’s Park wa chini ya miaka -18, Darryl Carrick, baada ya kumfuatilia kiungo huyo wa kati wa Scotland mara kadhaa msimu huu. (Team Talk)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here