TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO 31-07-2024
Borussia Dortmund wanakaribia kumnunua Pascal Gross wa Brighton, Romelu Lukaku wa Chelsea akubali kukatwa mshahara ili kuhamia Napoli, The Blues na Aston Villa wamewasilisha ofa kwa Maximilian Beier.
Chelsea wanajadili mpango wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, kujiunga na Napoli, huku mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, akitarajiwa kuhamia klabu hiyo kwa mkopo. (Athletic – usajili unahitajika)
Lukaku tayari amekubali kukatwa mshahara na kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Serie A. (Ben Jacobs)
Brighton wamekubali mkataba wa pauni milioni 5.9 kumruhusu kiungo wa kati wa Ujerumani Pascal Gross, 33, kujiunga na Borussia Dortmund. (Guardian)
Chelsea na Aston Villa wamewasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Maximilian Beier, 21. (Sky Germany)
Uhamisho wa Monza kwa mlinda mlango wa Nottingham Forest na Costa Rica Keylor Navas, 37, unaweza kutibuka kutokana na tofauti kati ya pande hizo mbili wakati wa mazungumzo. (Fabrizio Romano)
Chelsea pia wamefikia mkataba wa pauni milioni 16.7 na Genk kwa ajili ya mlinda mlango wa Ubelgiji Mike Penders, 18. (HLN – kwa Kiholanzi)
West Ham wako wanataka kujiondoa katika kinyang’anyiro cha kumnunua winga wa Leeds ya Uholanzi Crysencio Summerville, 22. (Talksport)
Aston Villa wanavutiwa na mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 27. (Express)
Everton wanafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Roma Muingereza Tammy Abraham, 26. (Sportitalia)
Manchester United wanajitahidi kufikia makubaliano na kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye aliondoka Juventus msimu huu wa joto. (Caughtoffside)
Beki wa England chini ya miaka 21 Rhys Williams, 23, na mlinzi wa Ufaransa Billy Koumetio, 21, wanatarajiwa kuondoka Liverpool. ((Athletic)
Liverpool wanapanga kusajili kiungo mkabaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa Agosti. (Football Insider)
Manchester United wanatarajiwa kusajili mbadala wa Scott McTominay , 27, iwapo watakamilisha mauzo ya kiungo huyo wa kati wa Scotland huku Fulham wakipanga kuwasilisha ofa mpya. (Football Insider)