UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa upo tayari kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Aprili 5 2024 nchini Misri.
Tayari kikosi cha Simba kimewasili Misri ilikuwa mapema Aprili 3 ambapo walipata muda wa kufanya mazoezi mepesi na Aprili 4 wanatarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo.
Ipo wazi kwamba mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-1 Al Ahly hivyo kazi kubwa ni kupata ushindi kusonga mbele hatua ya nusu fainali.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema wapo kamili kuwakabili wapinzani wao kwenye mchezo huo muhimu.
“Tunakwenda kufanya kazi ambayo wengi wameshasahau kwamba tunaweza kuifanya kupata matokeo kwenye mchezo mgumu na wa ushindani mkubwa hizo ni hesabu zetu.
“Ni mchezo mgumu lakini tunatambua umuhimu wake hivyo tutapambana kupata matokeo kimataifa, mashabiki wazidishe dua,”.