Simba Ahmed Ally kariakoo dabi

Kikosi cha Simba jana kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Cairo International, Misri, Aprili 5.

Wekundu hao wa Msimbazi watahitaji kupata ushindi wa zaidi ya bao moja ili kuingia hatua ya nusu fainali.

Akizungumza, Ofisa Habari wa klabu hiyo Ahmed Ally amesema jana wameanza mazoezi na hakuna majeruhi zaidi ya Aishi Manula ambaye aliumia akiwa na kikosi cha Taifa Stars kwenye michuano ya Fifa Series.

“Kikosi kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly. Wachezaji wote isipokuwa kipa Aisha Manula wako kwenye hali nzuri kiafya.

Tumeanza matayarisho ya mchezo huu mapema lengo likiwa kuingia nusu fainali,” amesema Ahmed.

Mara ya mwisho Simba kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ilikuwa mwaka 1974 ambapo ilifungwa na Mehalla El Kubra ya Misri kwa penalti 3-0 baada timu kushinda mchezo wa nyumbani kwa bao 1-0.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here