UONGOZI wa Simba umebainisha kwamba hesabu zao bado zipo palepale kufanya vizuri kwenye mechi zao kwa kuwa bado kuna nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi.
Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 19 vinara ni Yanga wenye pointi 52.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa ili kufanikiwa malengo ya kutwaa ubingwa wa ligi ni muhimu Wanasimba kuiunga mkono timu yao ili iweze kuchukua ubingwa wa NBC Premier League.
Ahmed ameyasema hayo alipozungumza na mashabiki wa timu hiyo mkoani Singida ambako leo watakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Ihefu ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili kwenye ligi.
“Simba Sports Club tunayo nafasi ya kuchukua ubingwa kwa kuwa kuna mechi ambazo zipo mkononi tunapaswa kupata matokeo na muhimu kwa Wanasimba kuwa pamoja.
“Tuna mchezo dhidi ya Ihefu tunatambua ni mchezo mgumu lakini tupo tayari tunahitaji kupata matokeo mazuri,”.
Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Simba ni pamoja na Luis Miquissone, Kibu Dennis.