AZAM FC matajiri wa Dar wametoshana nguvu dhidi ya Mashujaa kutoka Kigoma, mwisho wa reli katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Baada ya dakika 90 ubao umesoma Azam FC 0-0 Mashujaa kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.
Azam FC inasalia nafasi ya pili ikiwa na pointi 51 Mashujaa nafasi ya 14 pointi zao kibindoni ni 22 zote zimecheza mechi 23.
Matokeo mengine Aprili 17 2024 ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa Namungo 1-0 Coastal Union, Uwanja wa Majaliwa na mtupiaji bao la ushindi alikuwa ni Hassan Kabunda dakika ya 8.
Tabora United 0-3 Kagera Sugar watupiaji wakiwa ni Moubarack Amza dakika ya 24, Obrey Chirwa dakika ya 48 na Mbaraka Yusuph dakika ya 72 mchezo huu ulichezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.