KITAIFA

MASIKINI LAWI AREJEA BONGO, HATIMA YAKE HAIJUI

Baada ya kurejea nchini, beki Lameck Lawi amesema hatma ya yeye kuitumikia Coastal Union ipo chini ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya Simba kuendelea kukomaa.

“Nipo nchini, kwa sasa siwezi kuzungumza chochote kuhusiana na mambo yaliyotokea Ubelgiji, kikubwa ninachoweza kusema naendelea kujifua na Coastal Union, kuhusiana na kucheza sijajua hatma yangu hadi sasa,

“Tangu nimerudi nipo pamoja na Coastal Union lakini mambo bado hayajakaa vizuri kwenye suala la Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambapo ndio kesi ipo huko, hivyo mambo yakienda sawa nitacheza.

Lawi ambaye alisaini mkataba ndani ya Simba, ameshindwa kuitumikia timu hiyo na badala yake alitimkia Ubelgiji kwa ajili ya kujaribu kwenye klabu ya K.A.A Gent lakini mambo yameenda tofauti, hivyo amerudi Tanzania

Lawi akizungumzia namna mchakato wake wa usajili ulivyoenda amesema anapitia wakati mgumu sasa kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kuendeleza alipoishia msimu uliopita na hatimaye kufikia malengo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button