Uongozi wa klabu ya Simba Uongozi umemteua Kocha Juma Mgunda kukinoa kikosi cha Simba akisaidiwa na Selemani Matola hadi hapo Bodi ya Wakurugenzi itakapotoa uamuzi mwingine.
Hatua hiyo imekuja baada klabu hiyo kuvunja mkataba na aliyekuwa Kocha wa kikosi hicho,
Abdelhak Benchikha pamoja na wasaidizi wake wawili Kamal Boujnane na Farid Zemit.
Juma Mgunda ataanza kazi katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC utakaochezwa April 30, Ruangwa Mkoani Lindi katika Uwanja Majaliwa.