WAPINZANI wa Simba, Mashujaa Fc kwenye mchezo wa leo Uwanja wa Lake Tanganyika, Mashujaa wamekataa unyonge mbele ya Mnyama kwa kubainisha kwamba wamefanya maandalizi mazuri kuwakabili.
Leo Aprili 9 Simba wanakuwa wageni mbele ya Mashujaa mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kusaka ushindi ndani ya dakika 90.
Kocha Mkuu wa Mashujaa, Mohamed Abdallah,(Bares) ameweka wazi kuwa anatambua mpinzani wake namna alivyo imara kutokana na kushiriki mashindano ya kimataifa lakini wamejiandaa vizuri.
“Simba wameonyesha kiwango kizuri kimataifa hilo tunalitambua licha ya kwamba wameondolewa katika mashindano hayo. Sisi tumejipanga kwa hilo katika mashindano haya”.
“Tumekuwa na muda mzuri wa maandalizi na sasa tunakwenda kufanya kazi yetu uwanjani licha ya kwamba hali ya hewa imekuwa ngumu kuturuhusu kufanya mazoezi kwa asilimia kubwa uwanjani, tupo tayari,”.