Simba

Aliyekuwa kocha wa viungo wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, Adel Zrane amefariki dunia leo nchini Rwanda.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo leo, umetoa pole kwa familia na timu ya APR ya Rwanda na wadau wote.

Kocha huyo alijiunga na Simba msimu wa mwaka 2018 na kuondoka 2021 katika benchi la ufundi la timu hiyo.

“Zrane alikuwa mtu mkarimu sana, mcheshi na rafiki kwa wachezaji, alipendwa na kila mmoja,” imeeleza taarifa hiyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here