Rasmi Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limeweka wazi kuwa kila klabu itakayoashiriki mashindano ya kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu itapata kiasi Cha Pesa €50 milioni sawa na shilingi bilioni 137 za kitanzania.
Huku klabu ambayo itatwa ubingwa wa michuano hiyo itavuna kiasi cha €100M sawa na shilingi bilioni 275 pamoja na kombe la michuano hiyo.
Kutoka EPL (Uingereza) ni timu mbili pekee ndizo zitashiriki michuano hiyo,Chelsea na Manchester City ambazo zitaungana na vilabu vingine 8 kutoka shirikisho la UEFA huku CAF ikipeleka jumla ya vilabu 4.