Simba

KUGOTEA hatua ya robo fainali kwa Simba msimu wa 2023/24 ni kufeli kwa mara nyingine tena kwa kuwa hawajajifunza wakati wote walipofika hatua ya robo fainali.

Wakati wote nilikuwa nikibainisha kuwa haina maana kwamba Simba huwa wanakuwa hawana nafasi hapana wanashindwa namna ya kumaliza kazi nyumbani. Kufeli kwa Simba dhidi ya Al Ahly hesabu ziliharibikia nyumbani, Uwanja wa Mkapa walipopoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Nafasi walizopata zaidi ya 10 walizotumia hovyo, utulivu hakuna na eneo la ushambuliaji hapo mzigo umekuwa mzito. Mtego wa kutinga makundi wanaumudi ikitokea ikiwa tofauti pengine msimu ujao hata robo fainali hawatafika.

Al Ahly wanasonga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0 hili tatizo la ushambupiaji inabidi lifañyiwe kazi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here