Simba kuwafuata Ihefu

BAADA ya kukamilisha kete kwenye CRDB Federation dhidi ya Mashujaa ya Kigoma, Aprili 10 msafara wa kikosi cha Simba umeanza kuelekea Singida.

Ipo wazi kwamba Aprili 9 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ulisoma Mashujaa 1-1 Simba katika raundi ya nne na kupelekea mshindi kupatikana kwe penalti.

Mashujaa 6-5 Simba ilikuwa hivyo na kufanya kazi ya Simba kugotea hapo kwa wakati huu mpaka wakati mwingine kwenye mashindano hayo ambayo yana mdhamini mpya.

Kituo kinachofuata kwa Simba ni Aprili 13 itakuwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa walikuwa wanahitaji ushindi dhidi ya Mashujaa lakini haijawa hivyo kwao.

“Tulikuwa tunahitaji ushindi kwenye mchezo wetu dhidi ya Mashujaa bahati haijawa kwetu tunakwenda kujipanga upya kwa ajili ya wakati ujao na sasa nguvu tunazipeleka kwenye Ligi Kuu Bara,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here