Shabiki wa Simba SC, anayetambulika kwa jina la GB 64 ameitwa Kituo cha Kati (Central) kutoa Maelezo, huku akisema ana wasiwasi huenda akawekwa ndani ya kukosa kuitazama mechi dhidi ya Yanga SC.
Katika video inayotembea mitandaoni inaonesha shabiki huyo aliyejizolea umaarufu kwa kuikosoa timu yake ya Simba katika kipindi hiki ikionekana kuwa dhaifu.
GB 64 ameonekana akilalamika kuitwa kituoni hapo na huenda akakosa kulitazama pambano hilo litakalochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.