USHINDI wa Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu unawapa pointi tatu mazima huku mwamba Feisal Salum akifikisha mabao 14.
Azam FC wameituliza Ihefu kwenye mchezo wa ligi na kusepa na pointi tatu mazima ambazo zinawaongezea kasi kuufukuzia ubingwa wa ligi msimu wa 2023/24.
Ni dakika ya 13 alipachika bao hilo la ushindi ambalo lilidumu mpaka dakika ya 90 Uwanja wa Azam Complex.
Azam FC inafikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 24 ikiwaacha Simba kwa tofauti ya pointi 8 kwa kuwa Simba wana pointi 46 nafasi ya tatu.
Vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 58 baada ya kucheza mechi 22 msimu wa 2023/24.
Aziz KI ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao 15 na namba mbili ni Feisal mwenye mabao 14 msimu wa 2023/24.