Yanga

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga a kimataifa Yanga wapo ndani ya ardhi ya Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao zinazofuata kimataifa na kitaifa.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi imetinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na pointi 8 kibindoni.

Mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi ilipoteza pointi tatu ugenini dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Yanga ni pamoja na Dickson Job, Metacha Mnata, Djigui Diarra, Aziz KI.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema mpango mkubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zao watakazocheza kitaifa na kimataifa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here