KIMATAIFA
YANGA WAJIANDAE NI MWENDO WA KUWASHAMBULIA TU
Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rulani Mokwena amesema kuwa kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Yanga SC hatoingia uwanjani kwa dhumuni la kuzuia kwani yeye siyo muumini wa soka hilo
“Kwangu sijawahi kuutazama mchezo wa mpira wa miguu kwenye kujilinda zaidi bali nautazama mpira wa miguu kama burudani ambayo inapaswa kuambatana na matokeo mazuri, hakuna kitakachobadilika dhidi ya Yanga, kuhusu mbinu ni siri yangu na Wachezaji wangu, naamini tuna Kaka na Dada wengi tu hapa Tanzania ambao watakuja kutushangilia” amesema Mokwena