Leny Yoro

Unaambiwa beki bishoo Mfaransa mwenye kipaji cha ajabu Leny Yoro anayechezeae klabu ya Lille amekataa ofa kutoka klabu ya Mashetani Wekundu (Man United) huku yeye lengo lake ikiwa ni moja tu kusajiliwa na Real Madrid.

Man Utd tayari wamekubaliana na klabu ya Lille kuhusu usajili wa beki huyo kwa ofa yenye thamani ya zaidi ya €50m sawa na Tsh Bilioni 143.

Lille, wanamsisitizia Yoro kukubali kujiunga na Man Utd kwani ndiyo klabu iliyotoa ofa bora zaidi kwa sasa.

Leny Yoro yeye anaipa kipaumbele Real Madrid na anaendelea kutumaini Madrid wakubaliane na Lille. Na kwa upande wa Real Madrid wanataka kumsajili dogo kwa masharti yao wenyewe, na kama Lille watakataa basi Madrid wamesema wapo radhi kusubiria mpaka 2025 atakapomaliza mkataba kisha wamsajili kama mchezaji huru.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here